Highlights

Askofu Kivuva Musonde awataka Vijana kutambua na kutumia vipaji na talanta walizopewa na mungu kwa manufaa ya jamii

Na Silvio Nangori

Askofu mkuu wa Mombasa, Mhashamu Martin Kivuva Musonde, amewataka vijana kutambua na kutumia vipaji na talanta walizopewa na mungu kwa manufaa ya jamii, huku akiwaonya dhidi ya vishawishi vinavyoweza kuharibu mustakabali wao.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa 21 wa chama cha mabaraza ya maaskofu katoliki Afrika Mashariki (AMECEA), unaoendelea jijini Nairobi, Askofu mkuu Kivuva ameeleza namna Jimbo Kuu la Mombasa linavyotekeleza wito wa kuandamana na vijana katika safari yao ya maisha na imani.

Amesema kanisa linawatambua vijana kama nguzo muhimu ya jamii, hivyo lina wajibu wa kuwasikiliza, kuwaelekeza na kuwasaidia kufikia ndoto zao.

Amefichua kuwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, Jimbo Kuu la Mombasa limeteua mapadre watatu wenye jukumu maalum la kuwasindikiza na kuwaongoza vijana katika shughuli mbalimbali za kichungaji.

Post Comment