Highlights

Marsabit yaweka mikakati ya kukabiliana na majanga kabla ya msimu wa mvua za El nino

Na Joyce Akiny & JB Nateleng

Naibu gavana wa kaunti ya Marsabit, Solomon Gubo, amewataka washikadau wanaohusika na usimamizi wa majanga kuwasilisha taarifa sahihi kuhusu athari za mvua zilizopita, huku kamati ya kutathmini majanga (CSG) ikiendelea kukusanya ripoti za uharibifu wa miundombinu katika maeneo mbalimbali ya kaunti.

Akizungumza na wanahabari, Gubo amesema ni jukumu la kamati hiyo kubainisha kwa uwazi kiwango cha uharibifu uliosababishwa na mvua zilizopita na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kaunti kujiandaa kwa mvua zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi kijacho.

Gubo amesema ingawa baadhi ya wakulima walifanikiwa kupata mavuno katika msimu uliopita wa mvua, kiwango cha chakula kilichopatikana bado hakitoshelezi mahitaji ya wakazi wengi wa kaunti akisisitiza kuwa hatua za mapema zinahitajika ili kuimarisha usalama wa chakula.

Ripoti hiyo, inayoratibiwa na mamlaka ya kitaifa ya kusimamia ukame (NDMA) tawi la Marsabit, inatarajiwa kutoa tathmini ya kina kuhusu athari za mvua zilizopita na kuwasilishwa kwa serikali ya kitaifa ili kuwezesha kubuniwa kwa hatua za haraka za kukabiliana na dharura.

Post Comment