Polisi warejesha ngamia wanne walioibwa Laisamis,Marsabit.
Na Nyabande Orwa
Siku chache baada ya tukio la wizi wa idadi kubwa ya mifugo katika eneo la Gudas, Loglogo, eneo bunge la Laisamis, polisi wamefanikiwa kuwapata na kuwarejesha ngamia wanne.
Akizungumza na wanahabari, kamanda wa polisi wa kaunti ya Marsabit, Leonard Kimaiyo, amesema ngamia hao walipatikana katika eneo la Koya, pia katika eneo bunge la Laisamis. Katika tukio hilo, idadi isiyojulikana ya ngamia, mbuzi na ng’ombe waliibwa na watu wasiojulikana.
Wakati huo huo, kamishna wa kaunti ya Marsabit, Stanley Kamande, amewatahadharisha wakazi wa maeneo yaliyoathirika dhidi ya kujihusisha na vitendo vya kulipiza kisasi, akisisitiza kuwa vyombo vya usalama vinaendelea na uchunguzi ili kuwabaini na kuwakamata wahusika.



Post Comment