Viongozi wa Dukana wahimiza amani na kukomesha kisasi
Na Samuel Kosgei
Viongozi wa kijamii kutoka eneo la Dukana, katika eneo bunge la North Horr, wamezitaka jamii za eneo hilo kuishi kwa amani, kuvumiliana na kudumisha uhusiano mwema na jamii jirani.
Wakiongozwa na aliyekuwa MCA mteule, Kizito Konchora Abduba, viongozi hao wamesema kuwa jamii za Marsabit zinapaswa kuachana na vitendo vya kulipiza kisasi, wakisema tabia hiyo ndiyo chanzo kikuu cha migogoro ya mara kwa mara katika kaunti hii.
Konchora amesema kuwa panapotokea visa vya uhalifu, ikiwemo wizi wa mifugo, wananchi wanapaswa kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama ili wahusika wachukuliwe hatua, badala ya kuvamia au kulipiza kisasi dhidi ya jamii jirani.
Kauli yake inajiri siku chache baada ya shambulizi la wizi wa mifugo kutokea katika eneo la Gudas, Loglogo, kaunti ya Marsabit.
Aidha, Konchora amezitaka jamii zinazoishi katika wadi za Illeret na North Horr kuendelea kushirikiana na kuimarisha juhudi za kutafuta na kudumisha amani ya kudumu kati ya jamii hizo.



Post Comment