Highlights

Risasi 4060 zapatikana Moyale, polisi na jeshi kuziangamiza

Na Nyabande Orwa

Maafisa wa Polisi kwa ushirikiano na maafisa wa Jeshi la Kenya wanaendelea na mipango ya kuharibu risasi zilizopatikana jana katika mji wa Moyale.

Akithibitisha tukio hilo, kamanda wa polisi wa kaunti ya Marsabit, Leonard Kimaiyo, amesema kuwa risasi 450 zilipatikana na watu waliokuwa wakichimba msingi wa nyumba mkabala na shule ya upili ya Moyale Senior mjini Moyale. Baada ya ugunduzi huo, walitoa taarifa kwa vyombo vya usalama vilivyofika eneo hilo na kuanza uchunguzi.

Kimaiyo amesema inaaminika kuwa eneo ambako risasi hizo zilipatikana huenda lilikuwa ghala la silaha lililotumiwa na wanajeshi wakati wa vita kati ya Italia na Uingereza katika kipindi cha ukoloni.

Aidha, amewataka wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama wanapokutana na vitu vinavyotiliwa shaka ili vikaguliwe na wataalamu na kuepusha hatari inayoweza kujitokeza.

Post Comment