Highlights

Mabadiliko ya Tabianchi yatishia elimu ya watoto wa jamii za wafugaji Marsabit.

Naibu Gavana wa Marsabit, Solomon Gubo, amesema kuwa mabadiliko ya tabianchi yameibuka kuwa changamoto kubwa inayotatiza elimu ya watoto kutoka jamii za wafugaji kutokana na kuhamahama mara kwa mara kutafuta maji na malisho.

Akizungumza wakati wa uzinduzi ya wiki ya Siku ya Mtoto wa Afrika eneobunge la Saku, Gubo alisema kuwa uhaba wa maji unawalazimu wafugaji kuhama kutoka eneo moja hadi jingine wakisaka maji ya mifugo na ya matumizi ya nyumbani, hali inayosababisha watoto wengi kukosa masomo au hata kuacha shule kabisa.

Kauli hiyo imeungwa mkono na mtetezi wa haki za binadamu na Mkurugenzi wa Shirika la MWADO, Nuria Gollo, ambaye amesema kuwa ukosefu wa maji katika maeneo kadhaa ya Kaunti ya Marsabit umechangia ongezeko la wanafunzi wanaoacha shule na pia kuongezeka kwa visa vya dhuluma za kijinsia dhidi ya watoto.

Mratibu wa huduma za watoto katika ukanda wa mashariki Salome Muthama amekariri haja ya jamii za wafugaji kuwacha mila na tamaduni za kukeketa watoto na pia ndoa za mapema anayosema imefikia asilimia 31 katika kaunti ya Marsabit.

Post Comment