Highlights

Wanafunzi waanza mapumziko ya siku tano nchini

Na Nyabande Orwa

Wanafunzi kote nchini wameanza mapumziko ya katikati ya muhula wa pili leo Jumatano. Mapumziko hayo yatadumu kwa siku tano kuanzia Juni 24 hadi Juni 28, huku masomo yakitarajiwa kuanza tena Juni 29. Muhula wa pili unatarajiwa kukamilika rasmi Julai 31.

Mapumziko haya yanajiri wakati ambapo baadhi ya shule zimekumbwa na visa vya migomo na uchomaji wa mabweni, hali iliyosababisha usumbufu wa masomo na kufungwa kwa baadhi ya taasisi za elimu. Wizara ya Elimu imesema kuwa shule 204 zimeathiriwa na migomo hiyo, lakini idadi hiyo ni ndogo na haikuhitaji kufungwa kwa shule zote mapema.

Post Comment