Mwakilishi wa Baba Mtakatifu ahimiza kanisa kuendeleza maendeleo Jumuishi ya binadamu
Mjumbe maalum wa Baba Mtakatifu katika Kongamano la 21 la AMECEA, Mhashamu Kadinali Michael Czerny, ameongoza kikao cha pili cha siku ya pili ya kongamano hilo kwa kutoa hotuba iliyosisitiza dhamira ya Kanisa katika kukuza maendeleo jumuishi ya binadamu.
Kadinali Czerny, ambaye ni Mkuu wa Dikasteri ya Vatican ya Kukuza Maendeleo Jumuishi ya Binadamu, aliwasilisha salamu za Papa kwa wajumbe wa kongamano huku akihimiza Kanisa kuendelea kushuhudia Injili kupitia huduma zinazogusa utu, haki na ustawi wa watu.
Hotuba yake ilifungua mjadala uliolenga kutathmini historia ya AMECEA, maendeleo yaliyofikiwa tangu kuanzishwa kwake na mwelekeo wa baadaye wa Kanisa Katoliki katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Kongamano la 21 la AMECEA linaendelea katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki (CUEA), Nairobi, likiwakutanisha maaskofu na wajumbe kutoka nchi wanachama kujadili nafasi ya Kanisa katika kujibu changamoto za wakati huu na kuimarisha utume wake katika ukanda huo.



Post Comment