Featured Stories / News

WALIMU 289 WAAJIRIWA KAUNTI YA MARSABIT KWA KANDARASI YA KUDUMU

BARAZA la mitihani ya kitaifa KNEC limetakiwa kusikiliza kilio cha walimu wanaosimamia mitihani na hata wanaosahihisha mitihani ambao kwa muda sasa wamekuwa wakiitaka serikali kuwaongezea marupurupu kwenye malipo yao. Katibu wa chama cha kutetea maslahi ya walimu KNUT tawi la Marsabit, Rosemary Talaso, ameitaka baraza hilo kusikiliza kilio cha walimu[Read More…]

SEREKALI YA KAUNTI YA MARSABIT YATAKIWA KUWAPIGA JEKI VIJANA NA WANAWAKE ILI KUPUNGUZA KIWANGO CHA UMASKINI.

Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya kumaliza umaskini duniani,serekali ya kaunti ya Marsabit pamoja na ile ya kitaifa zimetakiwa kuwapiga jeki vijana na wanawake haswa walio katika sekta ya kilimo ili kupunguza kiwango cha umaskini katika kaunti ya Marsabit. Kulingana na mkurugenzi wa shirika la maendeleo endelevu, Initiative for Progressive Change[Read More…]

ASILIMIA 47.9 YA KAYA KATIKA KAUNTI NDOGO YA SAKU ZINAMILIKI VYOO.

Asilimia 47.9 ya kaya katika kaunti ndogo ya Saku zinamiliki vyoo na kuvitumia katika kuzuia utupaji wa kinyesi ovyo maarufu Open Defecation Free (ODF) Haya ni kwa mujibu wa afisa wa afya katika kaunti ndogo ya Saku Gobba Boru. Akizungumza kwenye hafla ya kuadhimisha siku ya usafi wa mkono duniani iliyoandaliwa katika[Read More…]

Arbe Roba Gocha na Leah Lesila wafanya vyema katika mashindano ya Nondo Desert Wheel Chair yaliyoandaliwa mnamo siku ya jumamosi kaunti ya Isiolo.

Afisa mkuu katika idara ya utamaduni na jinsia kaunti ya Marsabit Anna Maria Denge amewapongeza Arbe Roba Gocha na Leah Lesila ambao walipeperusha bendera ya Marsabit kwenye mashindano ya watu wanaoishi na ulemavu ya Nondo Desert Wheel Chair yaliyoandaliwa mnamo siku ya jumamosi katika kaunti ya Isiolo. Arbe Roba Gocha[Read More…]

Wito wa kujisajili kwenye bima ya afya ya SHIF wazidi kutolewa.

Huku mabadiliko makubwa kwenye mamlaka ya afya ya jamii (SHA) yakizidi kushuhudiwa kimfumo, wananchi wametakiwa kuzidi kujisajili ili kuweza kupokea matibabu katika hospitali mbalimbali jimboni Marsabit. Meneja wa bima ya (SHIF) eneo pana la Saku, North Horr na Laisamis, Mutuma Kaaria amewataka wananchi kuzidi kujiandikisha wao na familia zao ili[Read More…]

JAMII IMETAKIWA KURIPOTI VISA VYOVYOTE VYA KUTILIWA SHAKA AMBAVYO VINAWEZA PELEKEA MAFUNZO YA ITIKADI KALI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT.

Jamii imetakiwa kuripoti visa vyovyote vya kutiliwa shaka ambavyo vinaweza pelekea kuwepo kwa mafunzo ya itikadi kali katika kaunti ya Marsabit. Kwa mujibu wa ACC wa Marsabit Central Martin Buluma ni kuwa jamii ifaa kuripoti visa vya watu kutoweka ili kuhakikisha kuwa idara ya usalama inafuatilia na kuzuia wao kupewa[Read More…]

Subscribe to eNewsletter