Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
WAKULIMA waliotayarisha mashamba yao na kupanda katika eneobunge la Saku kaunti hii ya Marsabit imeongezeka kwa asilimia 25 mwaka huu kulingana na idara ya kilimo kaunti ndogo ya Marsabit Central.
Afisa wa kilimo kaunti ndogo ya Saku Duba Nura ameambia shajara kuwa idadi kubwa ya wakulima walitayarisha mashamba yao msimu huu mvua wa mvua fupi za Oktoba, November na December.
Japo mvua zimechelewa kunyesha, Nura anasema kuwa tayari mimea iliyopandwa imemea na wakulima wana matumaini ya kupata mazao.
Kwa wale ambao waliogopa kupanda kutokana na mvua kuchelewa, Nura amewaambia wasichoke kwani mimea inayokuwa kwa muda mfupi kama vile mboga au mtama inafaa kupandwa ili isaidie katika kuhakikisha usalama wa chakula jimboni.
Wakulima katika eneo la Dakabaricha viungani mwa mji wa Marsabit wameonesha Imani kuwa watapata chakula cha kutosha iwapo mvua itazidi kunyesha mwezi ujao.
Aidha wamewataka vijana kujihusisha na kilimo kwani ndio njia rahisi ya kujiajiri kwa sasa.