Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Wakaazi wa Marsabit wametoa hisia tofauti kuhusu uwezo wa akina mama nchini kuwania urais na kushinda kiti hicho.
Miongoni mwa akina mama wanaotarajiwa kuwania urasi katika uchaguzi wa mwaka wa 2027 ni kinara wa chama cha narc kenya Martha Karua.
Wakizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee baadhi ya wakaazi wa mji Marsabit wamesema wakati wa akimama kushinda kiti cha urais bado haujafika ikizingatiwa bado nchi ni changa kwenye suala la demokrasia.
Aidha wengine wameshikilia kuwa mila na utamaduni ya taifa bado haiamini akinama kuweza kuongoza ikizingatiwa safari ndefu ya ukomavu wa kisiasa.
Hata hivyo baadhi ya wakaazi wamesema ya kwamba Martha Karua anatosha kuwania urais kwa sababu tangu Kenya kupata uhuru taifa haijapiga hatua kubwa sana hivyo wangependa akina mama pia wajaribiwe.