Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Jamii ya Marsabit imetakiwa kuhakikisha kwamba watoto wanoishi na ulemavu na wamo katika umri wa kudhuria masomo wamepelekwa shuleni.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri ni kwamba idara yake imebaini kuwa kuna idadi kubwa ya watoto wanaoishi na ulemavu katika kaunti ya Marsabit ambao bado wamo manyumbani.
Akizungumza na Idhaa hii kwa njia ya kipekee Magiri amewarai wazazi waliona watoto wanaoishi na ulemavu kuhakikisha kwamba wanawapa haki yao ya kimsingi ya kupata elimu ili waweze kujifaidi katika siku za usoni.
Aidha Magiri ameahidi kuwa idara ya elimu itafanya msako kuhakikisha kwamba watoto wote wanaoishi na ulemavu na wamo katika umri wa kuhudhuria masomo wanapelekwa shuleni wakati shule zitakapofungulliwa kwa muhula wa kwanza mwezi januari mwaka ujao wa 2025.
Kadhalika mkuu huyo wa elimu jimboni ameirai jamii ya Marsabit kuasi unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na ulemavu na badala yake kuwakubatia na kuwashirikisha katika mipangilio mbalimbali ya kijamii.