WANANCHI MARSABIT WASIFU KANISA KWA KUKATAA MCHANGO WA WANASIASA NCHINI.
November 19, 2024
County updates, notifications, news from the Marsabit County
Wazazi katika kaunti ya Marsabit wameshauriwa kutolegeza kamba kwa wanao haswa msimu huu wa likizo ili kuzuia wasichana kupata mimba za utotoni. Kwa mujibu wa afisa wa watoto katika kaunti ya Marsabit, Abudho Roba ni kuwa baadhi ya mimba za mapema kwa wasichana zinaweza epukika iwapo wazazi watatekeleza majukumu yao[Read More…]
Wahudumu wa afya wa kujitolea CHPs katika eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit wametishia kuandamana iwapo serekali ya kaunti haitawalipa mishahara yao wa miezi minne. Baadhi ya waliozungumza na Shajara ya Radio Jangwani wametaja kuwa hawajapokea mishahara ya mwezi Julai,Agosti,Septemba na Oktoba mwaka huu. Wametaja kwamba hilo linalemaza kazi[Read More…]
Idadi ya vijana wanaoambukizwa virusi vya Ukimwi kaunti ya Marsabit inazidi kuongezeka. Haya ni kwa mujibu wa mtetezi wa watu wanaoishii na virusi vya ukimwi jimboni Marsabit Mwalimu Qabale Tache. Akizungmza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee, Qabale amesema kuwa hali hiyo imechangiwa na ukosefu wa hamsa[Read More…]
UCHIMBAJI wa migodi katika eneo la Hillo eneobunge la Moyale utasalia kufungwa na kuingia eneo hilo kwa saasa ni kinyume cha sheria. Onyo hilo limekaririwa na Collins Ochieng ambaye ni mwanajiolojia katika kaunti ya Marsabit. Akizungumza na idhaa hii ofisini mwake Ochieng amesema kuwa ikiwa mgodi huo ungekuwa unafanya kazi[Read More…]
Baadhi ya wakaazi wa Marsabit wamepewa mafunzo kuhusu namna ya kutumia meko ya kisasa kupikia chakula ikiwa ni lengo mojawapo ya taifa la Kenya kufikia asilimia 100 ifikapo 2028 katika kupika na meko yenye kukabili hewa chafu. Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee afisini mwake mkurugenzi mkuu katika[Read More…]
Mtihani ya kitaifa ya gredi ya sita KPSEA umeongo’a nanga rasmi hii leo huku wanafunzi wakikalia mtihani wa Hesabu na kingereza. Kwa mujibu wa mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri ni kuwa ni jumla ya watahiniwa 8,383 wa shule za msingi ambao wamekalia mtihani huo katika vituo vya[Read More…]
Wakaazi wa kaunti ya Marsabit wamesifia matumizi ya mitandao katika jamii kwa kusema kuwa inasaidia kuwaunganisha na wapendwa wao na kuwajuza yanayojiri katika maeneo tofauti duniani. Baadhi ya waliozungumza na Shajara Ya Radio Jangwani, wamesema kuwa mtandao unasaidia pakuwa katika kuelimisha jamii na kuwataatharisha kuhusiana na mabadiliko ya tabia nchi[Read More…]
Vijana wa kaunti ya Marsabit wametoa hisia zao kuhusiana na ukosefu wa ajira. Baadhi ya waliozungumza na Shajara ya Radio Jangwani, wamelalamikia kuwa ukabila na ufisadi ndio kikwazo kikuu katika upatikanaji wa ajira hapa nchini. Wamesema kuwa idadi kubwa ya watu wanaajiriwa kwa misingi ya kabila huku wakihisi kutengwa kutokana na[Read More…]
Mwenyekiti wa shirikisho la mpira wa miguu FKF tawi la Marsabit Mohamed Nane amekanusha madai kuwa amejiuzulu na kujiondoa katika kinyanganyiro cha mweyekiti wa shirikisho hilo kwenye uchaguzi mkuu wa Disemba 11 mwaka huu. Akizungumza na Radio Jangwnai kwa njia ya simu, Mohamed Nane ameutaja uvumi huo kama propaganda zinzoenezwa[Read More…]
Chama cha kutetea maslahi ya walimu (KNUT) tawi la Marsabit kimechagua mwalimu Kula Lula Omar kuwa mwenyekiti wake mpya kwenye uchaguzi mdogo ulifanyika mjini Marsabit siku ya Jumamosi. Kula sasa anajaza nafasi hiyo iliyoachwa wazi na mumewe aliyeaga dunia mwanzoni mwa mwaka Huu. Nafasi hiyo ilikuwa imevutia wagombeaji wawili ambao ni Kula[Read More…]