Local Bulletins

Baadhi ya wakaazi wa Marsabit wamtaka Raila Odinga kustaafu baada ya kupoteza uchaguzi wa AUC….

Na Henry Khoyan

Siku chache baada ya kinara wa ODM Raila Odinga kupoteza kwenye uchaguzi wa kuwania nafasi ya uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), baadhi ya wakaazi wa Jimboni wametoa hisia zao kuhusiana na hatua za kisiasa ambazo waziri mkuu huyo wa zamani anafaa kuchukua.

Wakaazi hao wamemtaka kiongozi huyo kustaafu na kuondoka katika siasa za nchi.

Wameeleza wazi kuwa huu ni wakati muafaka kwa Odinga kuachia ngazi ya uongozi na kuwaruhusu viongozi wengine kuchukua madaraka.

Subscribe to eNewsletter