WAZAZI MARSABIT WAHIMIZWA KUTOWAFICHA WATOTO WALIO NA ULEMAVU WA KUPOOZA KWA UBONGO MAARUFU CELEBRAL PALSY.
November 4, 2024
Huku baadhi ya wakaazi jimboni Marsabit wakilalama ukosefu wa chakula, serikali inatarajiwa kuzindua mradi wa kukabiliana na ukame katika maeneo ya kaskazini mwa nchini yaani Drought Resilience Programme in Northern Kenya, hapo kesho katika kaunti ndogo ya Sololo kaunti ya Marsabit.
Kulingana na mratibu wa mradi huo Daniel Odero aliyezungumza na shajara ya Radio Jangwani, mradi huo unaotarajiwa kutekelezwa katika kaunti ya Marsabit na Turkana, na utaendeshwa na serikali ya Kenya kwa ushirikiano na serikali ya Ujerumani huku ukifadhiliwa na benki ya KFW kutoka ujerumani.
Kenya itapokea mkopo wa shilingi bilioni moja ili kuendesha mradi huo.
Mifugo watanufaika zaidi kutokana na mradi wa lishe kwa mifugo yaani feedlots ambao unatarajiwa kuendeshwa chini ya mradi huo wa kukabiliana na ukame huku wananchi wakinufaika na maji.
Vilevile Odero amedokeza kuwa wanalenga kunufaisha wakaazi 255,000 kutokana na miradi mbalimbali itakayofanikishwa chini ya mradi huo.
Kwa upande wake waziri wa kilimo katika kaunti ya Marsabit Hussein Ali Fundi ameutaja mradi huo kama hatua kubwa kwa wafugaji na wakulima katika kuimarisha maisha yao haswa baada kaunti ya Marsabit kupoteza zaidi ya asilimia 75 ya mifugo wao katika kipindi cha ukame.