Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
regional updates and news
NA SAMUEL KOSGEI Chama cha ODM kinachoongozwa na Raila Odinga kinaitaka serikali ya Kenya Kwanza kuwajibikia mauaji, majeruhi na utekaji nyara ulioshuhudiwa nchini kufuatia maandamano ya Gen Z kupinga mswada tata wa fedha. Katika taarifa iliyosomwa na katibu mkuu wake Edwin Sifuna jijini Nairobi chama hicho kimeendelea kukashifu maafisa wa[Read More…]
NA SAMUEL KOSGEI Walimu wa shule za chekechea katika kaunti ya Marsabit wamepokezwa mafunzo ya kidijitali hatua ambayo inalenga kuwafaa wanafunzi 11 katika kaunti ndogo zote za Marsabit. Afisa mkuu katika idara ya elimu kaunti ya Marsabit Qabale Adhi alisema kuwa walimu wote wa ECDE watapokea mafunzo hayo ya kusomesha[Read More…]
Na Samuel Kosgei KAMPUNI ya kushughulikia masuala ya maji na majitaka kaunti ya Marsabit MARWASCO imeomba wakaazi wa mji wa Marsabit kuvumilia hatua ya maji kukatwa na kampuni hiyo siku nne zilizopita. Meneja mkurugenzi wa kampuni hiyo Sora Katelo akizungumza na wanahabari katika bwawa la Bakuli ulio mlima Marsabit Jumatatu[Read More…]
NA JOHN BOSCO NATELENG Kundi la Vijana kutoka eneo la Manyatta Ilman Chito wadi ya Sagant Jaldesa wametoa rai kwa serekali ya Kaunti kuwakarabatia barabara ambayo imetatiza uchukuzi katika eneo hilo. Galma Iya ambaye ni mmoja wa Vijana hao amesema kuwa watu wa eneo hilo wamekuwa wakitatizika na ubovu wa[Read More…]
Na Caroline Waforo Idara ya kilimo jimboni Marsabit imethibitisha kuwepo kwa nzige humu jimboni. Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani naibu mkurugenzi wa kilimo jimboni Hassan Charfi amethibitisha hilo japo anaeleza kuwa nzige hao ambao wameripotiwa katika maeneo mengi jimboni Marsabit ni ‘nzige-miti’ yaani tree locust na wala sio nzige[Read More…]
NA CAROLINE WAFORO Kulingana na afisa wa kufuatilia magonjwa ya mifugo jimboni Marsabit Dkt Bernard Chege ambaye amezungumza na shajara ni kuwa PPR ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoathiri haswa mbuzi na kondoo na umethibitishwa katika eneo pana la Chalbi ikiwemo Elbeso, Kalacha, Maikona, kati ya mengine. Dr Chege anasema[Read More…]
NA GRACE GUMATO Huduma za hospitali ya rufaa ya Marsabit zimelemezwa hii leo kutokana na kuandamana kwa wafanyikazi wa hospitali hiyo baaada ya kulalamika kuwa hawajalipwa mishahara ya mwezi mitatu. Aidha wanafanyikazi hao ikiwemo madaktari na wauguzi wa hospitali hawajalipwa kwa miezi mitatu huku wafanyikazi wasio wa kudumu wakidai hawajalipwa kwa[Read More…]
Na Samuel Kosgei Kuna haja ya kuendeleza hamasisho dhidi ya tabia ya kukeketea wasichana jimboni Marsabit na sehemu zote zinazofanya zoezi hilo dhalimu. Hayo ni kulingana na bodi ya kitaifa ya kupinga zoezi la ukeketaji nchini Anti FGM board. Mkurugenzi mkuu wa bodi hiyo kukabiliana na FGM nchini Bernadette Loloju amesema[Read More…]
Na Grace Gumato Mwanaume mwenye umri wa makamu ameshtakiwa kwa kosa la kumnajisi msichana mwenye umri wa miaka 15, katika mahakama ya Marsabit hii leo. Mshukiwa, Augustine Lekamurte amedaiwa kuwa mnamo tarehe 23 Juni mwaka huu katika mtaa wa Loiyangalani kaunti ya Marsabit alimnajisi mtoto wa miaka 15. Mshukiwa huyo[Read More…]
NA SAMUEL KOSGEI Jumla ya wabunge 195 wamepiga kura ya ndio kuunga mkono mswada tata wa fedha ambao umepokea pingamizi kubwa kutoka kwa umma huku huku wabunge 106 na wakipiga kura ya kuupinga. Kura tatu zikiharibika. Hatua hiyo ilijiri huku maelfu ya Wakenya wakiingia barabarani katika miji mbalimbali wakiandamana kupinga[Read More…]