Local Bulletins

MWANAUME MWENYE UMRI WA MAKAMU AMESHTAKIWA KWA KOSA LA KUMNAJISI MSICHANA MWENYE UMRI WA MIAKA 15, KATIKA MAHAKAMA YA MARSABIT HII LEO.

Na Grace Gumato

Mwanaume mwenye umri wa makamu  ameshtakiwa kwa kosa la kumnajisi msichana mwenye umri wa miaka 15, katika mahakama ya Marsabit hii leo.

Mshukiwa, Augustine Lekamurte amedaiwa kuwa mnamo tarehe 23 Juni mwaka huu katika mtaa wa Loiyangalani kaunti ya Marsabit alimnajisi mtoto wa miaka 15.

Mshukiwa huyo amefikishwa mbele ya hakimu mkuu Christine Wekesa na kukana mashtaka dhidi yake huku mahakama ikimwachilia kwa bondi ya shilingi 100,000 au mdhamini sawa na hiyo, kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tarehe 11 mwezi ujao mwaka huu.

Wakti uo huo Lotaba Elongot Apetet amefikishwa katika mahakama ya Marsabit leo hii kwa makosa mawili ikiwemo  kosa la kumnajisi mtoto mwenye umri wa miaka 15 na pia kumshika mtoto huyo kwa njia isiyofaa.

Mshukiwa huyo amefikishwa mbele ya hakimu Christine Wekesa na mahakama imeagiza kesi hiyo kuahirishwa mpaka tarehe 3 mwezi ujao  kwa sababu ya kukosekana kwa mkalimani wa lugha.

Subscribe to eNewsletter