Wito watolewa kwa wazazi kaunti ya Marsabit,kuwa karibu na wanao kipindi cha likizo fupi….
February 24, 2025
CHAMA cha kutetea maslahi ya walimu wa shule za msingi (KNUT) kimepinga mpango wa serikali kutaka kuwaajiri walimu wakuu wengine kuongoza madarasa ya gredi ya saba hadi tisa ilhali tayari shule husika tayari zina walimu wakuu. Akizungumza nasi kwa njia ya simu katibu wa chama cha walimu KNUT tawi la[Read More…]
Itakuwa ni afueni kwa waathiriwa wa dhulma za kijinsia jimboni Marsabit iwapo kituo cha uokoaji katika eneo la Log logo itafunguliwa. Kwa mujibu wa mwekahazina wa kundi la Isogargaro Women Group Hellen Ildhani ni kuwa kituo hicho kitasaidia katika kuwalinda watoto, pamoja na watu wazima ambao wanapitia dhulma za kijinsia,[Read More…]
Wakaazi katika kaunti ya Marsabit wamehimizwa kutotupa takataka ovyo ovyo bila idhini ya manispaa ya Marsabit. Ni hamasisho ambayo imetolewa na mkurugenzi katika manispaa ya mji wa Marsabit Boru Golicha. Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee golicha amesema wakati huu ambao msimu ya mvua unatarajiwa, kutupa taka ovyo[Read More…]
Waliokuwa wafanyikazi wa vibarua katika serikali ya kaunti ya Marsabit wamewasilisha kesi mahakamani kupinga kukatizwa kwa mkataba wao wa kazi. Walalamishi hao wanaojumuisha walinzi walioajiriwa kati ya mwaka 2014-2021 wanashutumu serikali ya kaunti ya Marsabit kwa kwenda kinyume na makubaliano na mkataba. Katika kesi hiyo iliyowasilishwa katika mahakama ya marsabit[Read More…]
|Idara Ya utabiri wa hali ya hewa ya kaunti ya Marsabit imesema kuwa Mvua za asubuhi pamoja na mvua za alasiri na hata usiku zinatarajiwa katika maeneo machache ya Kaunti katika kipindi cha wiki moja kuanzia tarehe 5 Jumanne hadi Jumatatu ijayo tarehe 11. Mkurugenzi wa idara ya hewa[Read More…]
ASKOFU wa kanisa la Kianglikana (ACK) kaunti ya Marsabit Wario Daniel Qampicha ameshutumu tabia ya wizi wa mitihani wa kitaifa akisema kuwa tabia hiyo hukuza jamii potovu iwapo haitakomeshwa. Askofu Qampicha akizungumza na radio jangwani kwenye kipindi cha Amkia Jangwani amesema kuwa kubembeleza tabia ya wizi wa mitihani ya kitaifa ni sawa[Read More…]
Viongozi wa kidini katika kaunti ya Marsabit wameunga mkono kauli ya rais William Ruto ya kuitaka jamii kuangazia kuhusu maadili mema kwa ajili ya kupunguza visa vya mauaji ya wanawake nchini. Akizungumza na idhaa hii, mchungaji wa kanisa la Redeemed Gospel hapa Marsabit Silver Savali ameelezea kuwa ni jukumu la[Read More…]
Hii ni kutokana na ripoti za upungufu wa damu katika hospitali ya rufaa ya Marsabit kutokana na hitaji la juu la damu. Ni wito ambao umetolewa na Christine Safia ambaye ni afisa wa benki la damu katika hospitali ya rufaa ya Marsabit. Akizungumza na shajara ya radio jangwani afisini mwake[Read More…]
Visa vya mimba za mapema vimetajwa kuwa sababu kubwa ya wasichana kukosa kwenda shule kote nchini kwa aslimia 39.2% huku asilimia 27.3% ikikosa kwenda shule kutokana na ukosefu wa karo. Kaunti ya Marsabit imetajwa pia kuwa kaunti mojawapo ya kaunti inayoshuhudia asilimia kubwa ya wanafunzi wasiohudhuria masomo kuanzia madarasa ya[Read More…]
KIJANA MOJA MWENYE UMRI WA MIAKA 22 AMEJITIA KITANZI MJINI MARSABIT. Kijana moja mwenye umri wa miaka 22 amejiua kwa kujitia kitanzi mjini Marsabit. Akithibitisha kisa hicho kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo amedokeza kuwa Kijana huyo alijitia kitanzi kutumia kamba katika eneo la Manyatta Willy viungani mwa[Read More…]