Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
CHAMA cha kutetea maslahi ya walimu wa shule za msingi (KNUT) kimepinga mpango wa serikali kutaka kuwaajiri walimu wakuu wengine kuongoza madarasa ya gredi ya saba hadi tisa ilhali tayari shule husika tayari zina walimu wakuu.
Akizungumza nasi kwa njia ya simu katibu wa chama cha walimu KNUT tawi la Marsabit Rosemary Talaso amesema kuwa kuajiri walimu wakuu wengine kuongoza madarasa mengine ya shule za msingi si sawa kwani itasababisha mzozo wa uongozi kati ya walimu wakuu wa zamani na wapya watakaoajiriwa.
Talaso amedai kuwa mpango wa serikali ni kuajiri walimu wakuu kutoka shule za sekondari.
KNUT sasa inaomba wizara ya elimu kuruhusu walimu wakuu wa shule za msingi kwa sasa waendelee kuongoza shule hizo kwani wana tajriba na pia itaepusha mgogoro ambao unanukia.
Aidha anasema hilo itasadia walimu hao kwani wataongezewa mishahara na marupurupu.