Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
|Idara Ya utabiri wa hali ya hewa ya kaunti ya Marsabit imesema kuwa Mvua za asubuhi pamoja na mvua za alasiri na hata usiku zinatarajiwa katika maeneo machache ya Kaunti katika kipindi cha wiki moja kuanzia tarehe 5 Jumanne hadi Jumatatu ijayo tarehe 11.
Mkurugenzi wa idara ya hewa kaunti ya Marsabit Abdi Dokata kwenye ripoti amesema kuwa dhoruba za radi zinatarajiwa kutokea katika baadhi ya maeneo ya kaunti.
Aidha amesema kuwa nusu ya pili ya kipindi cha utabiri huu kuna uwezekano wa kuwa na jua na ukavu.
Wastani wa Halijoto ya Juu Mchana anasema ni zaidi ya digirii 30 katika baadhi ya maeneo ya Kaunti haswa kaunti Ndogo za North Horr, Moyale na Laisamis.
Halijoto ya Wastani ya Wakati wa Usiku itakuwa ya Chini hadi digrii 17 hapa Saku na digrii 20 katika Kaunti Ndogo ya Moyale.
Kiwango cha juu zaidi cha mvua cha milimita 32.7mm kilirekodiwa ndani ya saa 24 katika mjini Moyale mnamo tarehe 3 Novemba 2024.