Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Waliokuwa wafanyikazi wa vibarua katika serikali ya kaunti ya Marsabit wamewasilisha kesi mahakamani kupinga kukatizwa kwa mkataba wao wa kazi.
Walalamishi hao wanaojumuisha walinzi walioajiriwa kati ya mwaka 2014-2021 wanashutumu serikali ya kaunti ya Marsabit kwa kwenda kinyume na makubaliano na mkataba.
Katika kesi hiyo iliyowasilishwa katika mahakama ya marsabit m,bele ya hakimu mkuu mwandamizi Christine wekesa Baadhi ya walalamishi wanadai kuchukua mikopo kwenye benki na hivyo imekuwa vigumu wao kulipa mkopo huo baada ya kuachishwa ajira.
Kandarasi ya Wafanyikazi hao wanane ilitarajiwa kukamilika terehe 1 disemba 2025 ila serikali ya kaunti ilikatiza kandarasi zao kutokana na kufikisha miaka 60 ambao ni umri wa kustaafu.
Kutokana na hayo walalamishi wanaitaka serikali ya kaunti kuwapa fidia ya mshahara wa mwaka nzima, malipo ya huduma ya miaka waliohudumu na Siku za likizo bila malipo fedha zinazojumuisha kati ya shilingi elfu 370 hadi elfu 600 kwa wanane hao.
Walalamishi hao wamesema kuwa serikali ya kaunti ya Marsabit haijaonyesha nia ya kusuluhisha malalamisha yao licha ya kutoa notisi ya kuelekea mahakamani.
Aidha hakuna mwakilishi yeyote wa serikali ya kaunti ya marsabit iliyefika mahakamani.
Hata hivyo kesi hiyo itatajwa tena tarehe 7 Januari mwaka 2025.