Local Bulletins

Raia 9 wa Eritrea na wawili Ethiopia wapigwa faini ya Sh50,000 au kifungo cha miezi 2 kwa kosa la kuwa nchini Kenya kinyume na sheria.

Raia 9 wa Eritrea wamepigwa faini ya shilingi elfu 50,000 au kifungo cha miezi 2 kwa kosa la kuwa nchini Kenya kinyume na sheria.

Hii ni baada ya tisa hao kufikishwa katika mahakama ya Marsabit mbele ya hakimu mwandamizi Simon Arome hapo jana Alhamisi ambapo walikiri mashtaka dhidi yao.

Mahakama hiyo imearifiwa kuwa siku ya  Alhamisi katika makutano ya Marsabit Kargi kaunti ndogo ya Marsabit Central raia hao tisa wa Eritrea walikamatwa wakiwa nchini bila stakabathi hitajika na kuwasilishwa mhakamani siku io hiyo.

Hakimu Arome ameagiza 9 hao kurejeshwa makwao baada ya kulipa faini au kutumikia kifungo.

Wana siku 14 kukata rufaa.

Raia wawili wa Ethiopia wamepigwa faini ya shilingi elfu 50 au kifungo cha miezi miwili kwa kuwa nchini kinyume na sheria.

Wawili hao walikamatwa hapo jana Alhamisi katika eneo la Ququ-fami kaunti ndogo ya Marsabit North kwenye barabara kuu ya Moyale-Marsabit na kuwasilishwa mahakamani leo hii mbele ya hakimu mwandamizi Simon Arome ambapo wamekiri mashtaka dhidi yao.

Wana siku 14 kukata rufaa.

Subscribe to eNewsletter