Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
KIJANA MOJA MWENYE UMRI WA MIAKA 22 AMEJITIA KITANZI MJINI MARSABIT.
Kijana moja mwenye umri wa miaka 22 amejiua kwa kujitia kitanzi mjini Marsabit.
Akithibitisha kisa hicho kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo amedokeza kuwa Kijana huyo alijitia kitanzi kutumia kamba katika eneo la Manyatta Willy viungani mwa mji wa Marsabit siku ya Jumamosi ya tarehe 2 mwezi huu wa Novemba.
Haijabainika kiini cha kijana huyo kujitia kitanzi.
Mwili wake umelazwa katika makafani ya hospitali ya rufaa ya Marsabit.
Wakati uo huo…
Watu watatu raia wa Ethiopia wamekamatwa humu jimboni Marsabit kwa kosa la kuwa humu nchini bila stakabadhi hitajika.
Kulingana na kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo, watatu hao wanaojumuisha wanaume wawili na mwanamke moja walikamatwa Jumatatu jioni baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Moyale kuelekea Nairobi kusimamishwa katika kuzuizi cha barabarani katika eneo la KBC kilomita kadha kutoka mjini Marsabit.