JAMII YA MARSABIT IMETAKIWA KUASI MBINU ZA KUKATA MITI NA KUCHOMA MAKAA ILI KUZUIA UHARIBIFU ZAIDI WA MAZINGIRA.
November 26, 2024
Na Caroline Waforo,
Wahudumu wa afya walio kwenye mgomo jimboni Marsabit wameombwa kusitisha mgomo wao na kurejea kazini huku mikakati ya kutafuta suluhu ikiendela.
Hii ni baada ya manesi jimboni kuanza mgomo wao rasmi hapo jana Jumatatu huku nao wahudumu wengine wa afya wanaojumuisha madaktari chini ya muungano wao wa KMPDU, maafisa wa kliniki chini ya mwavuli wa KUCO pamoja na wahudumu wa maabara wakipanga kuanza mgomo wao hivi karibuni baada ya makataa waliyoyatoa kwa serikali ya kaunti ya Marsabit kukamilika.
Akizungumza na Shajara Ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee katibu wa serikali ya kaunti ya Marsabit Hussein Tari Sasura amesema kuwa kuchelewa kwa mishara ya mwezi Julai Na Agosti ni kutokana na hatua ya serikali kuu kukosa kutuma mgao wa fedha kwa serikali za kaunti.
Wahudumu wa afya wamelalamikia kutowasilishwa kwa makato kwa taasisi husika swala ambalo katibu wa serikali ya kaunti anasema kuwa linachungunzwa baada ya kamati kuundwa kutekeleza hilo.
Aidha serikali ya kaunti ya Marsabit kupitia katibu wake imekana madai ya kuhujumu juhudi za wahudumu wa maabara kupata mwavuli wa kuwalinda katika kazi zao.
Kadhalika serikali imekana madai ya kuwa fedha za mshara wa mwezi Julai mwaka huu zilitumika kulipa mshahara wa mwezi Novemba 2023.
Na kuhusiana na kutolipwa kwa wanagenzi wa nyanjani maarufu interns kutoka idara mbalimbali katika serikali ya kaunti ya Marsabit Katibu Hussein Tari amewahakikishia kuwa watalipwa fedha hzio katika mwaka huu wa kifedha.
Hapo kesho washkadau kutoka serikali ya kaunti ya Marsabit itaandaa mkutano na wahudumu wa afya ili kujaribu kupata mwafaka.