Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Wanafunzi 126 waliosomea vyuo vya kiufundi jimboni Marsabit wameweza kuhitimu hii leo katika hafla ya kwanza iliyoandaliwa katika chuo cha kiufundi cha Saku, eneobunge la Saku, kaunti ya Marsabit leo Jumanne.
Akizungumza katika hafla hiyo, mke wa gavana wa Marsabit Alamitu Guyo amewataka mahafala hao kuweza kutumia ujuzi na ubunifu waliopata kuboresha maisha yao na pia jamii kwa ujumla.
Bi Alamitu amesema kuwa ni wajibu wa serekali kuwekeza Zaidi katika vyuo vya kiufundi ili kuwahimiza wanafunzi wengi kujiunga na vyuo hivi na kupata ujuzi utakaowafaidi.
Bi Alamitu amesema kuwa serekali kaunti ya Marsabit inazidi kujizatiti kusaidia vyuo vyote vya kiufundi jimboni hivyo kuwachangamoto vijana kushabikia mafunzo ya vyuo vya kiufundi.
Kadhalika amesema kuwa watashirikiana na washikadau tofauti ili kuhakikisha kuwa waliohitimu hii leo wamepokezwa vifaa ambavyo vitawasaidia katika kujiajiri.