Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Wakaazi katika kaunti ya Marsabit wameshauriwa kuhusu kupunguza kula mayai kupita kiasi.
Akizungumza na idhaa hii afisini mwake, mtaalamu wa lishe Regina Dorman amesema kuwa magonjwa kama kisukari yanaweza kuepukwa kwa kupunguza matumizi mengi ya mayai.
Alitahadhirisha kwamba ulaji wa mayai kwa kiasi ni muhimu lakini matumizi ya kupita kiasi yanaleta matatizo ya kiafya.
Aidha, amewarai kupunguza ulaji wa vyakula vya kisasa ili kujiepusha na magonjwa ya mtindo wa maisha bali wale lishe bora.
Pia amedokeza njia mwafaka wa kupika mayai ili kujiepusha na kula mafuta mengi kutokana na kupika mayai ya kukaaga.