Highlights

Wachuuzi wa maji Marsabit watoa makataa kwa kampuni ya MARWASCO

Na Nyabande Orwa

Wachuuzi wa maji mjini Marsabit, katika eneo bunge la Saku, wameipa kampuni ya usambazaji maji ya MARWASCO makataa ya siku mbili kuanza kusambaza maji, la sivyo wataandamana.

Wakizungumza na kituo hiki, wachuuzi hao wamesema kuwa Ijumaa iliyopita walikutana na uongozi wa kampuni hiyo, ambaye aliwahakikishia kuwa tatizo la ukosefu wa maji lingetatuliwa kufikia Jumatatu hii. Hata hivyo, wanasema hadi sasa hakuna mabadiliko yaliyofanyika.

Pia wamewalaumu baadhi ya viongozi wa kaunti kwa kile wanachodai ni uzembe katika kutekeleza majukumu yao, hali ambayo imeendelea kuwaathiri wakazi.

Wakati huo huo, wachuuzi hao wanasema wameanza kupata hasara kubwa ya kiuchumi kutokana na kusimama kwa shughuli za usambazaji wa maji, ambao ndio chanzo chao kikuu cha mapato. Aidha, wakazi wanaoishi katika nyumba za kukodi nao wameendelea kuathirika kutokana na uhaba huo wa maji.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment