Highlights

Wazazi watakiwa kuchukua jukumu la kulea maadili ya watoto

Na Nyabande Orwa

Mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu katika kaunti ya Marsabit, Rose Orguba, amewalaumu wazazi kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kuwalea watoto katika maadili mema.

Akizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu, Rose amesema kuwa jukumu la kuwafunza watoto maadili limeachiwa walimu pekee, ilhali wao wanapaswa kushughulikia masomo pamoja na nidhamu ya wanafunzi.

Amewataka wazazi kuchukua hatua madhubuti za kuwaongoza na kuwaadhibu watoto wao kwa njia inayokubalika, badala ya kuwaacha wakipotea kimaadili. Hata hivyo, amesisitiza kuwa adhabu hizo zisitumike kuvunja haki za watoto au kuwasababishia majeraha.

Matamshi yake yanajiri wakati ambapo baadhi ya viongozi wa upinzani wanaitaka serikali kuitisha mkutano wa wadau wa elimu na viongozi mbalimbali kujadili changamoto ya migomo ya shule nchini.

Cue in: Rose on adabu.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment