Highlights

Timu zitakazowakilisha Marsabit kwa mashindano ya shule za upili ukanda wa mashariki zabainika.

Na JB Nateleng

Timu zitakazoiwakilisha Kaunti ya Marsabit katika mashindano ya kanda ya shule za sekondari (KSSSA) zimebainika baada ya kukamilika kwa fainali za michezo ya kaunti.

Katika kandanda ya wasichana, shule ya Moi Girls Marsabit imetetea ubingwa wake na kufuzu kwa mara nyingine kuiwakilisha kaunti katika mashindano ya kanda.

Kwa upande wa voliboli ya wasichana, Moyale Girls pia imetetea taji lake na kujihakikishia nafasi ya kushiriki mashindano ya kanda nayo Moi Girls Marsabit imeendelea kung’ara katika netiboli kwa kutwaa ubingwa wa kaunti na kufuzu kwa mara nyingine kuiwakilisha Marsabit katika mashindano ya kanda yatakayofanyika wiki ijayo.

736455173_1260436432676959_7894480505503522825_n-1024x683 Timu zitakazowakilisha Marsabit kwa mashindano ya shule za upili ukanda wa mashariki zabainika.
Timu ya netiboli ya Moi Girls Marsabit ambao ndio mabingwa wa Netiboli Marsabit

Katika kandanda ya wavulana, Shule ya Sekondari ya Dakabaricha imerejea kwa kishindo baada ya kukosa ubingwa kwa miaka miwili, na sasa imetwaa taji la kaunti na kufuzu kuiwakilisha Marsabit katika mashindano ya kanda.

Kwa upande wa voliboli ya wavulana, Marsabit Mix imeendelea kudhihirisha ubora wake kwa kutwaa ubingwa wa kaunti na kujihakikishia tiketi ya kushiriki mashindano ya KSSSA ya kanda.

Timu hizo zitaiwakilisha Kaunti ya Marsabit katika mashindano ya Kanda ya Mashariki yatakayofanyika wiki ijayo katika Kaunti ya Makueni.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

2 comments

comments user
Barbara Jones

Very informative content, keep up the good work! Step end morning around on light.

comments user
Gita Utomo

Thanks for sharing such useful information. Language real home value usually leader be rise.

Post Comment