Highlights

Vijana zaidi  ya 1500 katika kaunti ya Marsabit  kupokea  mgao wa Nyota Fund  awamu ya pili.

Na Sabalua Moses

Zaidi ya vijana 1,500 katika kaunti ya Marsabit wamepokea  fedha za mpango wa Nyota, baada ya serikali ya kitaifa kuachilia mgao wa fedha hizo awamu ya pili hii leo kote nchini.

Akizungumza na wanahabari mjini Marsabit, katibu mkuu katika Idara ya usalama, Raymond Omollo, amesema kuwa zaidi ya wanufaika 1,500 kutoka kaunti hii watapokea fedha hizo, ambazo zinalenga kuwawezesha vijana kujiajiri na kuboresha maisha yao.

Kwa upande wake katibu mkuu katika wizara ya nishati na petroli Kello Harsame amesema kuwa vijana wanafaa kumakinika na kutumia ufadhili wa serikali ili kujinufaisha kimaisha.

Wakati uo huo naibu gavana katika kaunti ya Marsabi Solomon Gubo amesema serikali ya kaunti ya Marsabit itahakikisha kuwa vijana wanapata msaada katika kuendeleza biashara zao kupitia ufadhili wa Nyota Fund.

Post Comment