Viongozi wa kidini wakemea kisa cha mauaji ya mapacha Dukana, Marsabit
January 24, 2025
regional updates and news
Waliokuwa wafanyikazi wa vibarua katika serikali ya kaunti ya Marsabit wamewasilisha kesi mahakamani kupinga kukatizwa kwa mkataba wao wa kazi. Walalamishi hao wanaojumuisha walinzi walioajiriwa kati ya mwaka 2014-2021 wanashutumu serikali ya kaunti ya Marsabit kwa kwenda kinyume na makubaliano na mkataba. Katika kesi hiyo iliyowasilishwa katika mahakama ya marsabit[Read More…]
|Idara Ya utabiri wa hali ya hewa ya kaunti ya Marsabit imesema kuwa Mvua za asubuhi pamoja na mvua za alasiri na hata usiku zinatarajiwa katika maeneo machache ya Kaunti katika kipindi cha wiki moja kuanzia tarehe 5 Jumanne hadi Jumatatu ijayo tarehe 11. Mkurugenzi wa idara ya hewa[Read More…]
ASKOFU wa kanisa la Kianglikana (ACK) kaunti ya Marsabit Wario Daniel Qampicha ameshutumu tabia ya wizi wa mitihani wa kitaifa akisema kuwa tabia hiyo hukuza jamii potovu iwapo haitakomeshwa. Askofu Qampicha akizungumza na radio jangwani kwenye kipindi cha Amkia Jangwani amesema kuwa kubembeleza tabia ya wizi wa mitihani ya kitaifa ni sawa[Read More…]
Viongozi wa kidini katika kaunti ya Marsabit wameunga mkono kauli ya rais William Ruto ya kuitaka jamii kuangazia kuhusu maadili mema kwa ajili ya kupunguza visa vya mauaji ya wanawake nchini. Akizungumza na idhaa hii, mchungaji wa kanisa la Redeemed Gospel hapa Marsabit Silver Savali ameelezea kuwa ni jukumu la[Read More…]
Hii ni kutokana na ripoti za upungufu wa damu katika hospitali ya rufaa ya Marsabit kutokana na hitaji la juu la damu. Ni wito ambao umetolewa na Christine Safia ambaye ni afisa wa benki la damu katika hospitali ya rufaa ya Marsabit. Akizungumza na shajara ya radio jangwani afisini mwake[Read More…]
Visa vya mimba za mapema vimetajwa kuwa sababu kubwa ya wasichana kukosa kwenda shule kote nchini kwa aslimia 39.2% huku asilimia 27.3% ikikosa kwenda shule kutokana na ukosefu wa karo. Kaunti ya Marsabit imetajwa pia kuwa kaunti mojawapo ya kaunti inayoshuhudia asilimia kubwa ya wanafunzi wasiohudhuria masomo kuanzia madarasa ya[Read More…]
KIJANA MOJA MWENYE UMRI WA MIAKA 22 AMEJITIA KITANZI MJINI MARSABIT. Kijana moja mwenye umri wa miaka 22 amejiua kwa kujitia kitanzi mjini Marsabit. Akithibitisha kisa hicho kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo amedokeza kuwa Kijana huyo alijitia kitanzi kutumia kamba katika eneo la Manyatta Willy viungani mwa[Read More…]
Afisa mmoja anayesimamia mitihani katika shule ya mseto ya Ruso iliyoko katika kaunti ndogo ya North Horr amekamatwa hii leo kwa jaribio la kuiba mtihani wa KCSE inayoendelea. Akidhibitisha tukio hilo kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo amesema kuwa mshukiwa alikamatwa akipiga picha mtihani wa hesabu na kutuma[Read More…]
Wazazi Marsabit wahimizwa kutowaficha watoto walio na ulemavu wa kupooza kwa ubongo maarufu celebral palsy. Wazazi katika kaunti ya Marsabit wamehimizwa kutowaficha watoto walio na ulemavu wa kupooza kwa ubongo maarufu celebral palsy, hali ambayo huathiri ubongo wa mtoto, mama akiwa mja mzito. Ni hamasa ambayo imetolewa na mhudumu wa[Read More…]
Mwanaume mmoja auwawa katika kisa cha wizi wa mifugo,eneo la Loiyangalani kaunti ya Marsabit. Mtu moja ameuawa kwa kupigwa risasi huku mwingine akiachwa na majeraha ya risasi katika shambulizi la wizi wa mifugo katika eneo la Dakaiye wadi ya Loiyangalani kaunti ya Marsabit. Kulingana na kamanda wa polisi kaunti ya[Read More…]