JAMII YA MARSABIT IMETAKIWA KUASI MBINU ZA KUKATA MITI NA KUCHOMA MAKAA ILI KUZUIA UHARIBIFU ZAIDI WA MAZINGIRA.
November 26, 2024
Serikali ya kaunti ya Isiolo itatumia shilingi milioni 5 katika ujenzi wa makao salama RESCUE CENTRE kwa waathiriwa wa dhulma za kijinsia kwa ushirikiano na mamalka ya ujenzi wa barabara kuu nchini KENHA.
Haya yaliwekwa wazi na Nura Diba ambaye ni afisa wa masuala ya kijinsia katika kaunti ya isiolo aliyezungumza wakati wa siku ya kwanza ya maadhimisho ya siku 16 za kupigana na dhuluma za kijinsia ulimwenguni.
Na ili kuhakikisha kuwa kuna usawa wa kijinsia katika jimbo hilo la Isiolo Duba amesema serikali ya gavana Abdi Guyo imehakikisha kuna usawa wakati wa kuwaajiri wafanyikazi wa kaunti
Naye Caroline Leturupu ambaye ni kamishana katika tume ya masuala ya kijinsia nchini, alikashifu visa vyote vya dhuluma
Wakati wa hafla hiyo ilibainika kwamba kaunti ndogo ya Merti ndio inaongoza katika kaunti ya Isiolo kwenye idadi ya visa vya dhuluma ya kijinsia