SARATANI YA UMIO YATAJWA KUONGOZA KAUNTI YA MARSABIT KWA ASILIMIA 33.
November 27, 2024
Na Samuel Kosgei
Kaunti ya Marsabit imekuwa kaunti ya kwanza katika eneo pana la kaskazini kuzindua programu ya elimu ya dijitali kwa wanafunzi wa madarasa ya chekechea na walimu wao.
Kaunti ya Marsabit imekuwa kaunti ya kwanza katika eneo pana la kaskazini kuzindua programu ya elimu ya dijitali kwa wanafunzi wa madarasa ya chekechea na walimu wao.Meneja wa shirika la kutoa huduma za elimu kwa njia ya dijitali (EIDU) ukanda wa kaskazini Dalana Jarso amesema kuwa kufikia sasa wanafunzi 19,000 Marsabit wamepokea elimu ya dijitali huku walimu 540 pia wakipokea mafunzo hayo sawia.
Shule 360 za ECDE Marsabit zimepokea simu zilizo na mtaala Huo wa elimu ya dijitali.Dalana amesema kuwa katika ukanda huu wa kaskazini, shule za Marsabit zilitumika kwenye majaribio ya elimu hiyo ya dijitali na ametoa rai kwa walimu kuhakikisha kuwa wanafunzi wa ECDE wanafaidi na elimu hiyo ya kisasa.
Waziri wa elimu jimboni Marsabit Ambaro Abdulahi amesema kuwa ujio wa vifaa vya dijitali ni mfumo muhimu utakaobadilisha elimu ya watoto wa shule za chekechea.
Kwa upande wake gavana wa Marsabit Mohamud Ali amesema kuwa mpango huo wa elimu ya dijitali inafaa kukumbatiwa katika kaunti zote kwani inaendana mfumo wa sasa wa elimu na dunia ya sasa ya utandawazi.
Mohamud anasema baraza la kaunti za kaskazini imeshirikiana na shirika la EIDU na inalenga kufaidi wanafunzi elfu 150 wa madarasa ya chekechea.
Idara ya elimu ya ECDE pia imetabuliwa kwa kutekeleza hatua ya kuajiri walimu wa shule ya chekechea kwa kandarasi ya kudumu na yenye marupurupu yaani PnP.