Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Uchaguzi wa mashinani wa chama cha ODM umeanza rasmi leo katika kaunti ya Marsabit.Kwa mujibu wa mwenyekitiwa chama hicho tawi la Marsabit Ali Noor, ni kwamba uchanguzi huo umeng`oa nanga katika maeneo bunge yote manee ya kaunti ya Marsabit.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu, Noor amesema uchaguzi huu umeedamana na maagizo ya chama hicho ambayo yanamwataka kila mwanachama wao kumpigia kura mwenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu na mhasibu katika ngazi ya chini na baadae mwakani kufanya uchaguzi katika ngazi ya juu pia.
Noor ametoa wito kwa wakazi wa kaunti ya Marsabit kuzidi kujitokeza kujisajili kama wananchama wa chama hicho cha Chungwa na kupiga kura kwa njia ya haki na usawa.
Aidha Noor ameelezea kuwa kuna changmoto ya watu kujitokeza kutokana na hali ya mvua ambayo inashuhudiwa jimboni jambo ambalo limetatiza shughuli nzima ya uchaguzi huo.