Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Wito umetolewa kwa viongozi wa kisiasa kuasi kampeni za mapema na badala yake kuwajibikia manifesto ambazo waliahidi Wakenya wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.
Kwa mujibu wa mchungaji wa kanisa la PEFA hapa jimboni Marsabit Daudi Wako ni kuwa wanasiasa wanafaa kuasi kampeni za maapema ambazo zinaweza leta joto kali ya ukabila na chuki baina ya Wakenya.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee, Wako amesema kuwa viongozi wa kisiasa wanadeni la kuwafanyia Wakenya kazi badala ya kueneza propaganda ambazo haisaidii katika kuboresha uchumi wanchi.
Kiongozi huyu wa kidini, amesema kuwa ni muda muafaka kwa serekali kuweza kutimiza ahadi ambazo iliahidi Wakenya badala ya kuanza kampeni ambayo zinazorotesha uchumi na kufanya hali ya maisha kuwa ngumu zaidi.
Mchungaji Wako amewashauri viongozi wa kisiasa kuwekeza muda zaidi katika kusikiliza malalamishi ya wananchi na pia kuboresha sekta tofauti nchini ili kuwawezesha vijana pamoja na wananchi kufurahia maendeleo.