SARATANI YA UMIO YATAJWA KUONGOZA KAUNTI YA MARSABIT KWA ASILIMIA 33.
November 27, 2024
Na JB Nateleng
Ukosefu wa malezi mema katika kaunti ya Marsabit umetajwa kuchangia katika ongezeko la watoto wanaorandaranda mjini Marsabit.
Kwa mujibu wa mwalimu mkuu wa shule ya SKM Kame Koto aliyezungumza na meza ya habari ya Radio Jangwani ni kuwa ni sharti wazazi wajitwike jukumu la kuhakikisha kuwa wanajua kile ambacho wanao wanafanya ili kupunguza idadi ya wale ambayo wanarandaranda mtaani.
Mwalimu Kame amesema kuwa swala la kuhamasisha wazazi kuwapeleka wanao shuleni linafaa kuangaziwa upya ili kuhakikisha kuwa watoto wengi wamepelekwa shuleni.
Kadhalika Kame amesema kuwa ni sharti serekali ya kaunti na serekali kuu kubuni kituo cha marekebisho (Rehab Center) ili kuwasadia vijana ambao wameadhirika na mihadarati akisema kuwa hatua hiyo itasaidia katika kuwapa vijana elimu ambayo itawafanya wajirekebishe na kuishi Maisha mema.
Kauli yake iliungwa mkono na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya St John Boru Dabaso ambaye ametoa wito kwa walanguzi wa dawa za kulevya kukoma kuwapa watoto wadogo dawa hizi kwani wanaharibu kizazi kijacho.
Wakati huo huo, Fredrick Ochieng ambaye ni mwanaharakati wa kupambana na dawa za kulevya katika kaunti ya Marsabit amewarai wazazi kuwaheshimu wanao na kuwaelimisha vyema ili kuwafanya wawe watu wa kutegemewa maishani.