Highlights

Watu wenye ulemavu Marsabit wanufaika na vifaa vya kujikimu

NA Nyabande Orwa

Serikali kuu kupitia hazina ya watu wanaoishi na ulemavu imetoa vifaa vya kuanzisha biashara kwa watu 17 katika kaunti ya Marsabit.

Kulingana na afisa wa hazina hiyo, Isaac Alia, lengo ni kuwasaidia watu wanaoishi na ulemavu kujikimu kimaisha. Akizungumza na shajara Alia amesema mradi huu unaendelea katika maeneo ya Marsabit ya Kati na Moyale, ambapo watu wengine 30 wanatarajiwa kunufaika.

Katika hafla ya leo, walengwa wamepokea vifaa kama mashine za kuosha magari, mashine za kunyoa na vifaa vya saluni.

Wakati huo huo, hazina hiyo pia inasaidia shule za wanafunzi wanaoishi na ulemavu kwa kufadhili ujenzi wa madarasa.

Aidha, Isaac amewataka viongozi na wasimamizi kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kujisajili ili kunufaika na mpango huu.

Baadhi ya walionufaika wamesema msaada huo utawasaidia kujiendeleza kiuchumi, wakishukuru serikali kwa hatua hiyo.

Ali Adan, mkazi wa Moyale, ni mmoja wa wanufaika.

Mwenyekiti wa watu wanaoishi na ulemavu katika kaunti ya Marsabit, Doka Kuro, ameishukuru serikali kwa msaada huo.

Pia amewahimiza watu wenye ulemavu kujitokeza kwa wingi ili wanufaike na mipango ya serikali. Aidha, ameitaka serikali kuongeza juhudi za kuwasajili watu wa maeneo ya mashinani ili wapate vitambulisho.

Post Comment