Highlights

Mwanaume mmoja afungwa maisha gerezani kwa kumnajisi msichana wa miaka 8, Songa

Mahakama ya Marsabit imemhukumu kifungo cha maisha gerezani mwanaume mmoja kwa kosa la kumnajisi msichana mwenye umri wa miaka 8 katika lokesheni ya Songa kaunti ndogo ya Marsabit Central.

Lmeseku Lealo amepatikana na hatia ya kumnajisi msichana huyo mnamo tarehe 16 mwezi Februari mwaka 2025.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatano na Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya Marsabit Christine Wekesa.

Kwa mujibu wa mahakama, ushahidi uliowasilishwa ulithibitisha kuwa Lealo alitekeleza kosa hilo, huku ripoti ya kitabibu ikithibitisha kuwa mtoto huyo alinajisiwa.

Mhukumiwa ana siku 14 kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment