Highlights

Wananchi wa Saku wahimizwa kuchukua vitambulisho vyao vya kitaifa.

Na Abdiaziz Yusuf

Kiongozi wa vijana wa eneo bunge la Saku, Abdilaziz Boru, amewarai wakazi waliotuma maombi ya vitambulisho vya kitaifa kujitokeza kuvichukua ili kupunguza mrundikano wa vitambulisho ambavyo havijachukuliwa katika afisi za usajili.

Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani, Boru amesema baadhi ya vitambulisho hivyo hupelekwa katika afisi za machifu baada ya kutolewa, lakini bado wengi hawajajitokeza kuvichukua.

Aidha, amewahimiza wananchi watakaopokea vitambulisho vyao kujiandikisha kama wapiga kura ili waweze kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao na kutimiza haki yao ya kidemokrasia ya kuwachagua viongozi.

Wakati huo huo, Boru amemshukuru Rais William Ruto kwa kuondoa utaratibu wa kuwafanyia vijana wa eneo la Kaskazini Mashariki usaili maalum kabla ya kupatiwa vitambulisho vya kitaifa, akisema hatua hiyo imerahisisha upatikanaji wa stakabadhi hizo muhimu.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment