Highlights

Polisi wa Turbi waendeleza msako dhidi ya washukiwa wa uharibifu wa uzio wa shule

Na Nyabande Orwa

Polisi katika eneo la Turbi wanaendelea na msako dhidi ya zaidi ya vijana kumi wanaotuhumiwa kuhusika na uharibifu wa uzio wa shule ya Kukub Fami mapema Jumatano kufuatia mzozo wa mpaka.

Akizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu, OCPD wa Turbi, Daniel Mativo, amezionya jamii zinazoishi katika eneo hilo dhidi ya kujichukulia sheria mkononi pindi kunapotokea migogoro, akiwataka kutumia njia za kisheria kutatua tofauti zao.

Kauli yake inajiri siku moja baada ya mkurugenzi wa idara ya elimu ya jimbo katoliki la Marsabit, Padri Abraham Ali, kutoa wito kwa vyombo vya usalama kuharakisha uchunguzi na kuhakikisha washukiwa wanachukuliwa hatua za kisheria. Pia amesisitiza kuwa wanafunzi wa shule ya Kukub Fami waliokumbwa na tukio hilo wanapaswa kupata haki na mazingira salama ya kuendelea na masomo yao.

Post Comment