Highlights

Marsabit yajiandaa kuadhimisha siku ya vyama vya ushirika.

Na JB Nateleng

Huku dunia ikijiandaa kuadhimisha siku ya kimataifa ya vyama vya ushirika Jumamosi, Julai 4, kaunti ya Marsabit bado inakabiliwa na changamoto zinazokwamisha ukuaji wa vyama hivyo.

Akizungumza na wanahabari, waziri wa biashara, utalii na maendeleo ya vyama vya ushirika wa kaunti ya Marsabit, Jeremy Lendany, amesema kuwa ukubwa wa kaunti pamoja na uelewa mdogo wa baadhi ya wananchi kuhusu manufaa ya kujiunga na vyama vya ushirika ni miongoni mwa changamoto zinazoathiri maendeleo ya sekta hiyo.

Lendany amesema serikali ya kaunti, kupitia wizara yake, itaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku hiyo kwa shughuli mbalimbali zinazolenga kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa vyama vya ushirika katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Waziri huyo ameongeza kuwa maadhimisho hayo pia yataimarisha mshikamano na amani miongoni mwa jamii za Marsabit, yakiongozwa na kaulimbiu ya mwaka huu: Vyama vya Ushirika kwa Ajili ya Dunia Yenye Amani.

Post Comment