Highlights

Viongozi wa upinzani wakosoa mpango wa kituo cha karantini ya ebola Nanyuki

Na JB Nateleng

Viongozi wa upinzani, akiwemo Fred Matiang’i na Peter Munya, wameendelea kuikosoa serikali kuhusu mpango wa kujenga kituo cha karantini ya Ebola katika kambi ya Jeshi la Anga eneo la Nanyuki, Kaunti ya Laikipia County.

Wakizungumza hii leo kwa sauti moja viongozi hao wamesema mradi huo unapaswa kutathminiwa upya kwa kuzingatia masuala ya usalama wa jamii na uwazi katika maamuzi ya serikali, wakitaka mamlaka husika kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu utekelezaji wake.

Wamesisitiza umuhimu wa kuheshimu sheria na maoni ya wananchi kabla ya kuendelea na miradi ya aina hiyo inayohusisha afya ya umma.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment