Highlights

EACC yamtia mbaroni afisa wa jiji la Nairobi

Na JB Nateleng

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imemkamata Afisa Mkuu wa Kaunti ya Nairobi anayehusika na maendeleo ya miji na mipango, Patrick Analo Akivaga, kufuatia tuhuma za kupatikana na shilingi milioni 65.3 zilizofichwa katika mabegi wakati wa msako uliofanyika nyumbani kwake eneo la Syokimau, Kaunti ya Machakos.

Akizungumza na wanahabari baada ya kukamilisha msako huo mkurugenzi Mtendaji wa EACC Abdi Mohamed amesema msako huo ni sehemu ya uchunguzi unaoendelea kuhusu matumizi na uhalisia wa fedha hizo, huku hatua za kisheria zikitarajiwa kuchukuliwa baada ya uchunguzi kukamilika.

Abdi ameahidi kuendelea na juhudi za kupambana na ufisadi serikalini ili kuhakikisha kuna uwajibikaji na matumizi sahihi ya fedha za umma.

Post Comment