Highlights

Wazazi Marsabit wahimizwa kuimarisha malezi ili kukabiliana na utovu wa nidhamu shuleni

Na Sabalua Moses

Huku wimbi la vurugu likiendelea kushuhudiwa katika shule mbalimbali nchini, wazazi katika kaunti ya Marsabit wamehimizwa kutekeleza wajibu wa malezi ya wanao kikamilifu, ili kusaidia kukabiliana na ongezeko la visa hivyo vya utovu wa nidhamu.

Wito huu umetolewa na Naibu Kamishna Msaidizi katika kaunti ndogo ya Marsabit Central Richard Chepkonga aliyezungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika hapo jana Ijumaa katika shule ya msingi ya SKM.

Chepkwonga alisema kuwa wazazi wanapaswa kujenga maadili mema miongoni mwa watoto huku akisisitiza umuhimu wa mawasiliano ya mara kwa mara kati ya wazazi na watoto ili kutambua changamoto wanazokumbana nazo na kuwapa mwongozo unaofaa kabla hazijachangia mienendo isiyofaa shuleni.

Haya ni huku shule zaidi zikiendelea kufungwa kutokana na sintofahamu inayoshuhudiwa.

Shule ya upili ya Kakamega imewatuma wanafunzi nyumbani baada ya moto kuteketeza bweni.

Post Comment