Highlights

Miti milioni 30 kupandwa Badhauri kukuza uhifadhi wa mazingira

Msimamizi mkuu wa misitu katika kaunti ya Marsabit, Kenneth Muthuri, amesema idara yake kwa ushirikiano na serikali ya kaunti inalenga kupanda takriban miti milioni 30 katika eneo la Badhauri kama njia ya kurejesha misitu ya asili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza na kituo hiki wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, Muthuri amesema Marsabit bado iko nyuma katika kiwango cha uoto wa misitu, huku maeneo yenye misitu yakichukua asilimia 2.6 pekee ya eneo lote la kaunti. Ameeleza kuwa uchomaji wa makaa ndio chanzo kikuu cha uharibifu wa miti katika eneo hilo.

Muthuri amewataka wakazi kushirikiana na serikali katika juhudi za kuhifadhi mazingira kwa kushiriki kikamilifu katika upanzi wa miti, si tu kwenye maeneo ya umma bali pia katika makazi yao.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment