Mtu mmoja amefariki dunia baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani Marsabit
Mtu mmoja amefariki dunia baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani kwenye barabara kuu ya Moyale-Marsabit katika eneo la Parkishon.
Akithibitisha kisa hicho, OCPD wa Marsabit ya Kati, Beethoven Gachago, amesema inakisiwa kuwa marehemu, ambaye alikuwa akiendesha pikipiki kutoka Karare kuelekea Marsabit mjini, alipoteza mwelekeo wa pikipiki kutokana na upepo mkali uliokuwa ukivuma katika eneo hilo.
Gachago amesema kuwa marehemu alikuwa akisafiri peke yake wakati ajali hiyo ilipotokea. Uchunguzi kuhusu chanzo kamili cha ajali hiyo unaendelea.



Post Comment