Wanasiasa Marsabit watakiwa kuendesha siasa za amani kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027
Na Caroline Waforo
Wanasiasa wanaowania nyadhifa mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 katika kaunti ya Marsabit, wametakiwa kuendesha siasa za amani mshikamano na utangamano.
Wito huu umetolewa na Mratibu wa afisi ya msajili wa vyama vya kisiasa katika ukanda wa Mshariki ya Juu, Hassan Abdisalan, alipokuwa akizungumza leo Alhamisi katika warsha iliyolenga kukuza ushirikishwaji katika mchakato wa kisiasa na kuhimiza utoaji wa nafasi zaidi za uongozi kwa vijana.
Abdisalan amewataka wanasiasa kujiepusha na matamshi ya chuki na kauli zinazoweza kugawanya jamii huku taifa likielekea katika uchaguzi huo.
Wakati uo huo Abdisalan amehimiza vijana pamoja na wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania nyadhifa mbalimbali za uongozi ili kuhakikisha uwakilishi sawa katika uongozi na maamuzi ya maendeleo.



Post Comment