Highlights

Viongozi wa upinzani waitaka serikali kusikiliza wananchi kuhusu ujenzi wa karantini ya ebola

Na JB Nateleng

Hatua ya serikali ya kujenga kituo cha karantini ya Ebola imeendelea kuibua mjadala mkali nchini, huku viongozi mbalimbali wa kisiasa wakitaka maoni ya wananchi na maamuzi ya mahakama yaheshimiwe.

Akizungumza leo, Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro, amesema serikali ina wajibu wa kulinda maslahi ya wananchi na kuepuka kufanya maamuzi yanayokwenda kinyume na matarajio yao.

Nyoro pia ameitaka serikali kuheshimu agizo la mahakama lililosimamisha ujenzi wa kituo hicho hadi kesi iliyowasilishwa na Katiba Institute itakapokamilika kusikilizwa na kuamuliwa.

Aidha, mbunge huyo alisema serikali inapaswa kuelekeza nguvu zaidi katika kuboresha huduma za afya ya msingi kwa Wakenya badala ya kuwekeza katika miradi ambayo imezua utata, akionya kuwa hatua hiyo inaweza kuathiri vipaumbele vya sekta ya afya.

Naye Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, amesema fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha karantini ya Ebola nchini zinapaswa kuelekezwa kusaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuimarisha uwezo wake wa kukabiliana na ugonjwa huo.

Post Comment