Shule ya Upili ya Wasichana ya Bishop Cavallera kufunguliwa siku ya Jumamosi
Na Caroline Waforo
Shule ya Upili ya Wasichana ya Bishop Cavallera iliyoko Karare, eneobunge la Saku, kaunti ya Marsabit itafunguliwa siku ya Jumamosi ya tarehe 2 mwezi Mei mwaka 2026, kufuatia kufungwa kwake wiki iliyopita kutokana na kuripotiwa kwa ugonjwa usiojulikana miongoni mwa baadhi ya wanafunzi.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Mtawa Reginah Muthuku amesema kuwa usimamizi wa shule umeafikia uamuzi huo baada ya mashauriano na bodi ya shule, Wizara ya Elimu pamoja na ile ya Afya.
Aidha maombi maalum yataandaliwa shuleni siku ya Jumamosi ambapo wazazi pamoja na washikadau wote wamehimizwa kuhudhuria.
Ameeleza kuwa kabla ya shule kufunguliwa zoezi la upuliziaji dawa litafanyika hapo kesho Jumatano, chini ya usimamizi wa maafisa kutoka wizara ya Elimu na ile ya Afya.
Mtawa Muthuku ameongeza kuwa hakuna ugonjwa uliobainika kufuatia uchunguzi wa sampuli zilizochukuliwa na taasisi ya Utafiti wa Matibabu nchini KEMRI.
Itakumbukwa kuwa wanafunzi shuleni humo hasa wale wa kidato cha nne, wamekuwa wakishinikiza kufunguliwa kwa shule hiyo ili waweze kurejea masomoni bila kuchelewa zaidi



Post Comment