Radi yaua ngamia wanne Dukana kufuatia ya mvua kubwa
Na JB Nateleng
Ngamia wanne wamefariki baada ya kupigwa na radi katika kaunti Ndogo ya Dukana, eneo bunge la North Horr, Kaunti ya Marsabit kufuatia mvua kubwa iliyonyesha ikiambatana na ngurumo kali za radi usiku wa kuamkia leo Jumanne.
Kulingana na Chifu wa Dukana Tuye Katelo, tukio hilo liliripotiwa katika vijiji vya Dakabaricha na Dololo Boji, ambapo ngamia watatu waliuawa Dakabaricha huku mmoja akiuawa Dololo Boji.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu, chifu Katelo amesema hakuna mtu aliyepoteza maisha.
Aidha ametoa wito kwa wakazi kuchukua tahadhari wakati wa mvua zinazoambatana na radi ili kulinda maisha yao pamoja na mifugo



Post Comment